RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Monday, October 21, 2013

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NYONGEZA MWAKA 2013/2014

 MAELEKEZO MUHIMU:

Wanafunzi waliochaguliwa Orodha ya nyongeza kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa kuanzia Jumapili tarehe 22/09/2013 hadi 29/09/2013.
Fomu ya maelekezo (joining instruction) zinapatikana kwenye tovuti hii kwa kubofya hapo chini.
Wanafunzi wanatakiwa kufika Vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

 
1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania kidato cha NNE;
2. Ada ya muhula wa kwanza sh. 100,000/= au ya mwaka sh. 200,000/=;
3. Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya Chuo husika; na
4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.

 
Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.
Usajili wa kujiunga na Vyuo utafungwa tarehe 29/09/2013 saa 12.00 jioni


GRADE A 2013 Nyongeza
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA NYONGEZA MWAKA 2013/2014
MAELEKEZO MUHIMU:
 
Wanafunzi waliochaguliwa Orodha ya nyongeza kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa kuanzia Jumapili tarehe 22/09/2013 hadi 29/09/2013.
Fomu ya maelekezo (joining instruction) zinapatikana kwenye tovuti hii kwa kubofya hapo chini.
Wanafunzi wanatakiwa kufika Vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania kidato cha NNE na cha SITA;
2. Ada ya muhula wa kwanza sh. 100,000/= au ya mwaka sh. 200,000/=;
3. Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya Chuo husika; na
4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.

Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.
Usajili wa kujiunga na Vyuo utafungwa tarehe 29/09/2013 saa 12.00 jioni

icon DIPLOMA-ALPHABETI 2013 Nyongeza (105.93 kB)

| Print |
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUPATA SKOLASHIPU KWA MPANGO WA KUBADILISHANA WANAFUNZI KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA YA MSUMBIJI MWAKA 2014

Wanafunzi 51 wa Kitanzania wamechaguliwa kujiunga na masomo mbalimbali nchini Msumbiji katika ngazi ya Shahada ya Kwanza kupitia Mpango wa Kubadilishana Wanafunzi kati ya Serikali ya Tanzania na ya Msumbiji (Tanzania – Mozambique Students Exchange Programme – TAMOSE). Masomo yanatarajiwa kuanza juma la Kwanza la Januari, 2014.

Wanafunzi hao ambao orodha yao na masomo watakayosoma vimeambatishwa, wanatakiwa kufika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Idara ya Elimu ya Juu, Chumba Namba 28 kwa ajili ya maelekezo na maandalizi ya safari.

Wanafunzi hao wafike Wizarani kuanzia tarehe 30 Septemba hadi 14 Oktoba 2013 kuanzia Saa 3.00  asubuhi hadi saa 9:30 mchana katika siku za kazi.

Wanafunzi wanashauriwa kufika na nyaraka za kuombea pasi ya kusafiria nje ya nchi – passport (kwa wale ambao hawana). Nyaraka hizo ni pamoja na Cheti cha Kuzaliwa, Picha 5 za passport size zenye rangi ya buluu ya bahari pamoja na gharama za kuombea hati ya kusafiria nje ya nchi Wizara ya Mambo ya Ndani. Kwa wenye passport wanatakiwa kuja nazo.

icon List of Selected Students for Mozambique Scholarships 2014 (38.78 kB)


WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO MAALUM YA UALIMU (BRIDGING COURSE) MWAKA 2013/2014


MAELEKEZO MUHIMU
Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo haya wanatakiwa kuripoti Chuo cha Ualimu Morogoro kuanzia tarehe 18/10/2013 hadi 20/10/2013.

Wanafunzi wanatakiwa kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
  1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania vya Kidato cha NNE na SITA;
  2. Ada ya muhula wa kwanza sh. 100,000/= ;
  3. Sare ya Chuo (Suruali/sketi: koti na tai nyeusi; shati ya mikono mirefu ya rangi ya bluu bahari); na
  4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.
Usajili wa waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo utafungwa terehe 20/10/2013 saa 12.00 jioni.


icon WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO MAALUM YA UALIMU (2013/2014) (109.92


MADA ZITAKAZOFUNDISHWA NA KUTAHINIWA MWAKA WA KWANZA WA MASOMO KWA WANACHUO WA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA KUANZIA MWAKA 2013/2014

Ili kutekeleza Waraka wa Elimu namba 3 wa mwaka 2013, Wizara imeainisha mada zitakazofundishwa na kutahiniwa mwaka wa kwanza wa masomo kwa wanachuo wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada. Kila mkuu wa Chuo, Wakufunzi pamoja na Wanachuo wote wa mwaka wa kwanza wa kila Chuo wanaelekezwa kuzingatia maelekezo hayo ili kufanikisha utekelezaji wa Waraka husika.

icon Mada zitakazofundishwa na kutahiniwa mwaka wa kwanza wa masomo ngazi ya cheti na stashahada (107.03 kB)
NOTICE TO SUCCESSFUL LOAN APPLICANTS FOR 2013/2014 ACADEMIC YEAR  
The Higher Education Students’ Loans Board is hereby announcing names of successful first time loan applicants for 2013/2014 Academic Year who applied and were eligible for student loans.
The list includes the Institution to which the student is admitted to and the amounts of loans allocated to a particular student in all or part of the loanable items as per Guidelines and Criteria for Issuance of Loans and Grants for 2013/2014 Academic Year.
Loan applicants can access their loan status by keying in their Form Four Index Numbers to view the results.
Loan applicants are reminded that the loan money will be sent to their respective institutions where they will be required to sign to acknowledge receipt of the loans, after registration processes.
Issued by:
The Executive Director
Higher Education Students’ Loans Board
P. O. Box 76068