RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Burudani

RICK ROSS KUTUMBUIZA JUKWAA LA FIESTA OCTOBA 06, 2012



Rick Ross

Rick Ross

























Msanii nyota kutoka nchini Marekani, mzaliwa wa nchini  Marekani, anayetambulika kwa jina la kisanii kama Rick Ross, ambaye kwa jina halisi anajulikana kama William Leonard Roberts II, anatarajia kutua nchini Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kushiriki kikamilifu kushambulia jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, litakalofanyika Oktoba 6 ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa bin sawia kwa kila idara kuhusiana na tamasha hilo, waandaaji ambao ni Prime Time Promotions Ltd wakishirikiana na Clouds Media Group huku mdhamini wao mkubwa ikiwa ni kampuni ya bia ya Serengeti,wameandaa shamara shamra mbalimbali za kuhakikisha tamasha hilo mpaka linafika kileleni,linaamsha na kuacha gumzo la kipekee kabisa miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake, ikibidi mpaka Kigoma mwisho wa reli kwa namna moja ama nyingine.

Msanii huyo mwenye umahiri mkubwa wa kufloo awapo jukwaani mpaka sasa anatamba na nyimbo/albamu kadhaa kama vile  Hold Me Back 2012 God Forgives, I Don't, Hustlin' 2006 Port of Miami Diced Pineapples 2012 God Forgives, I Don't So Sophisticated 2012 God Forgives, I Don't 911 2012 God Forgives, I Don't Stay Schemin 2012 Rich Forever Aston Martin Music. 

Nyinginezo ni  2010 Teflon Don DJ Khaled 2008 Trilla Lemme See 2012 So Sophisticated Amsterdam 2012 God Forgives, I Don't Black Magic 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire The Boss 2008 Trilla You the Boss 2011 You the Boss Touch'n You 2012 Touch'N You Bag of Money 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire.
 
REDDS MISS TANZANIA 2012 KUFANYIKA NOV 03 UBUNGO PLAZA


Salha Israel (kulia) akifurahia zawadi yake ya gari aina ya Jeep wakati akikabidhiwa mwaka jana chini ya wadhamini wa waliopita kampuni ya huduma za simu ya Vodacom. Shindano hilo sasa linadhaminiwa na bia ya Redds.

Salha Israel (wa pili kushoto) akifurahia zawadi yake ya gari aina ya Jeep wakati akikabidhiwa mwaka jana chini ya wadhamini wa waliopita kampuni ya huduma za simu ya Vodacom. Shindano hilo sasa linadhaminiwa na bia ya Redds.

Salha Israel akiwa katika bango la Redds Miss Tanzania 2012 wakati wa uzinduzi wa shindano la mwaka huu


SHINDANO la Redds Miss Tanzania 2012 litafanyika Novemba 3 kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, waandaaji kamati wa Miss Tanzania wametangaza leo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, amesema warembo wataingia kambini Oktoba 2 katika hoteli ya Giraffe, ambako watakaa hadi siku ya shindano.
  
Mshindi wa shindano hilo atamrithi, Salha Israel kutoka Ilala anayeshikilia taji la taifa. Kwa kushinda shindano hilo mwaka jana, Salha alizawadiwa gari kali aina ya Jeep.

Hata hivyo, mapema mwaka huu kamati hiyo iliendesha shindano dogo na kumpata Lissa Jensen ambaye aliwakilisha nchi katika fainali za Dunia kutokana na mabadiliko ya kalenda yaliyofanywa na Kamati ya Miss World.

Miss Tanzania atakayepatikana Novemba 3 atakuwa na muda mrefu wa kujiandaa na atashiriki katika shindano la Miss World la mwakani na utaratibu huo utakuwa wa kudumu.

Hadi sasa, Miss Tanzania aliyepata mafanikio katika shindano hilo la dunia ni Nancy Sumary ambaye alitwaa taji la Miss World Africa 2005. 


SERENGETI FIESTA 2012-IRINGA



















KANYE WEST KUMFANYIA SHEREHE YA KUZALIWA (BIRHDAY) KIM KARDASHIAN KWA DOLLA MIL 1

Kim Kardashian akiwa na Kanye West











Rapa wa muziki wa Marekani Kanye West amepanga kutumia dolla za kimarekani milioni moja($1million) sawa na paundi (£615,000)katika sherehe ya kuazimisha kuzaliwa mpenzi wake Kim Kardashian mwezi ujao.Kanye pia amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na familia ya Kim kwa wiki kadhaa zilizopita kuhakikisha mipango inakwenda sawasawa.Katika sherehe hiyo Kim Kardashiani atakuwa akiadhimisha kutimiza miaka 32.

KANYE WEST AZIDI KUONEKANA KATIKA MATEMBEZI NA KIM KARDASHIAN
Kanye West akiwa na Kim Kardashian

ALIYEKUWA MMOJA WA MATOA HUDUMA MAARUFU WA MASHINDANO YA MAGARI YA FORMULA ONE AFARIKI DUNIA
Sid Watkin





Mtaalamu wa Uingereza aliyeboresha sana mashindano ya magari ya Formula One Sid Watkin amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.Sid Watkin ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Ayton Senna amejihusisha na Fornula One kwa muda wa robo karne sasa,akisaidia kuokoa maisha ya madereva wengi kama Rubens Barrichello na Mika Hakkinen kufuatia ajali ya mwendokasi.
''Hii ni siku ya huzuni sana kwetu na jamii yote ya michezo'' alisema rais wa FIA Jean Told
RIHANNA AIBUKA TENA NA CHRISS BROWN: AMUIGA KUVAA MENO YA DHAHABU

Waimbaji Rihanna(kushoto) na Chriss Brown(kulia) kwa nyakati tofauti

Baada ya mwimbaji Chriss Brown kuvaa meno ya dhahabu siku za hivi karibuni,mwanamziki mwenzake na ambaye pia alikuwa mpenzi wake,Rihanna naye amejitokeza hadharani akiwa amevaa meno ya dhahabu.Hali hilo imezua uvumi mwingi ikiwa labda Rihanna bado anampenda Chriss Brown.

No comments: