RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Wednesday, November 6, 2013

SERIKALI YAWEWESEKA NA ''ZIRO'' YAKE
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mh. William Lukuvi

KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kuweweseka kwa serikali katika sakata la kufuta daraja sifuri katika mitihani ya kidato cha nne na sita, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, jana alilazimika kumkana Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome.
Lukuvi alisema taarifa aliyoitoa Mchome wiki iliyopita kuwa serikali imefuta daraja sifuri kwa kidato cha nne na sita haikuwa ya serikali, bali ile iliyotolewa juzi na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, kuwa haijafutwa ndiyo sahihi.
Lukuvi alitoa kauli hiyo mara baada ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), kuomba mwongozo wa Spika akitaka kujua hatua watakazochukuliwa mawaziri wa wizara hiyo kwa kulidanganya Bunge na umma.