RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Saturday, November 2, 2013

WARIOBA ATAKA ELIMU CHUO KIKUU IBORESHWE


Rais wa Umoja wa waliokuwa wanafunzi wa Chuo Kkuu cha Dar es Salaam, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amewataka wahitimu wa chuo hicho kuungana kukisaidia kuboresha miundombinu na ubora wa elimu.

Jaji Warioba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema hayo juzi wakati umoja huo walipokutana kujadiliana jinsi ya kuboresha chuo hicho kwa kutoa michango yao pasipo kusubiri jukumu hilo kufanywa na Serikali.

Warioba alisema hali ya chuo ni ngumu kutokana na kuchakaa kwa miundombinu mbalimbali, uhaba wa walimu na vitendea kazi, jambo ambalo aliwataka kuunganisha nguvu kusaidia mabadiliko.

“Tukishirikiana tutahakikisha tunawasaidia wanafunzi wetu, pia michango yetu itaboresha elimu na kuleta mabadiliko,” alisema Jaji Warioba aliyesoma chuoni hapo miaka 50 iliyopita. Alisema tangu umoja huo ulipoanzishwa, zaidi ya Sh 2bilioni zimekusanywa na zote zimeelekezwa katika uboreshaji wa elimu chuoni hapo.

Akifafanua, Warioba alisema Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliandaa chakula cha jioni nchini humo, ambapo zaidi ya Sh350 milioni zilipatikana na kuahidi kuchangia zaidi sambamba na Rais Jakaya Kikwete.

Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga alisema lengo la chuo ni kuwashirikisha wahitimu kurudisha fadhila kwa kuchangia katika kuboresha seka ya elimu chuoni hapo.

Profesa Luoga alisema kutokana na chuo hicho kuwa kikongwe na kuzaa vyuo vingine nchini, jakumu kubwa kwao ni kuhakikisha wanavisaidia vyuo hivyo kufikia malengo yao.
Chanzo: Mwananchi

No comments: