RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Tuesday, August 14, 2012

UCHAMBUZI WA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 2012/2013


1. MIKOPO YA ELIMU YA JUU
Idadi ya wanafunzi waliopata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imeongezeka kutoka wanafunzi 91,568 mwaka 2010/11 hadi wanafunzi 93,176, mwaka 2011/12.

2. ONGEZEKO LA VYUO VIKUU NCHINI
Vyuo Vikuu vitatu (3) vilianzishwa ambavyo ni: Eckenford Tanga University, Jomo Kenyatta University of Agriculture na University of Bagamoyo; na Vyuo Vikuu vishiriki vitatu (3) vilianzishwa ambavyo ni: Jordan University College; St. Francis University College of Health and Allied Sciences; na St Joseph College of Engineering and Technology.

3. ONGEZEKO LA UDAHILI WA WANAFUNZI-NGAZI YA SHAHADA
Wizara ilifanikiwa kuongeza udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Elimu ya Juu kutoka wanafunzi 139,638 (wanawake 49,959) mwaka 2010/11 hadi wanafunzi 166,484 (wanawake 60,592) mwaka 2011/12. Hili ni ongezeko la asilimia 19. Aidha, idadi ya wanafunzi madaktari wa binadamu, meno na tiba ya mifugo iliongezeka kutoka 1,750 mwaka 2010/11 hadi 1,900 mwaka 2011/12.

4. ONGEZEKO LA UDAHILI WA WANAFUNZI-NGAZI YACHETI NA STASHAHADA
Wizara ilidahili jumla ya wanachuo 37,698 katika ngazi ya Cheti na Stashahada. Hili ni ongezeko la asilimia 2.9 ukilinganisha na idadi ya wanachuo 36,648 waliodahiliwa mwaka 2010/11 ambapo, walimu 292 kati ya hawa ni wa fani ya Elimu ya Michezo.

5. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA
(a) Udahili katika Vyuo vya Ufundi Stadi na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vinavyotoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi uliongezeka kutoka 102,217 (wanawake 50,190) mwaka 2010 hadi 121,348 (wanawake 56,849) mwaka 2011, ambalo ni ongezeko la asilimia 27; Vyuo vya Elimu ya Ufundi (Technical Education and Training) vilivyosajiliwa viliongezeka kutoka 224 mwaka 2010 hadi kufikia Vyuo 260 mwaka 2012.

(b) Udahili wa wanachuo katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali uliongezeka kutoka wanachuo 36,648 (wanawake 16,597) mwaka 2010 hadi 43,258 (wanawake 18,898) mwaka 2012.

(c) Idadi ya Vyuo Vikuu iliongezeka kutoka 34 mwaka 2010 hadi 46 mwaka 2012; na udahili wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu uliongezeka kutoka wanafunzi 139,638 (wanawake 87,778) mwaka 2010/11 hadi kufikia 166,484 (wanawake 60,592) mwaka 2011/12.

(d) Idadi ya wanafunzi waliopatiwa mikopo kwa ajili ya Elimu ya Juu iliongezeka kutoka 91,568 mwaka 2010/11 hadi kufikia 93,176 Mwaka 2011/12; Aidha, Wizara ilianza mfumo wa kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application System – OLAS).


Source: Hotuba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi 2012/2013

No comments: