RESEARCH AD

RESEARCH AD

CLEARING AND FORWADING

CLEARING AND FORWADING

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

THE GUARDIAN LTD

Saturday, November 2, 2013

SERIKALI KUSOMESHA BURE WANAFUNZI WA UDAKTARI 

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipo katika mchakato wa kuhakisha wanafunzi wote wanaochukua masomo ya Shahada ya Kwanza ya Udaktari kwenye vyuo binafsi na mashirika ya kidini wanagharamiwa bure na Serikali. Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi,alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Rita Mlaki(CCM).

Mbunge huyo alisema Jiji la Dar es Salaam lina takriban watu milioni tano na wote hukimbilia kupata huduma katika Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke.
Alihoji ni lini Serikali itawalipia ada wanafunzi wote wanaochukua shahada ya udaktari hata wale wanaosoma katika vyuo binafsi ikiwamo Chuo cha IMTU ili kuongeza idadi ya madaktari.


Akijibu swali hilo,Dk Mwinyi alisema kuna upungufu wa asilimia 45 ya madaktari nchini na kwamba Serikali inasomesha zaidi ya madaktari 13,000 kupitia vyuo mbalimbali nchini.
Pia Dk Mwinyi alisema, Serikali inaongeza bajeti kila inavyowezekana na sasa wanaandaa mpango wa kuwasomesha bure wanafunzi wanaosomea shahada ya kwanza ya udaktari katika vyuo binafsi na vya mashirika ya dini.
Hivi karibuni kumekuwapo na malalamiko ya kuwapo kwa upungufu mkubwa wa madaktari katika hospitali mbalimbali nchini.

Chanzo: Mwananchi

No comments: