ZITTO KABWE : UBUNGE SASA BASI!
Zitto Kabwe na Joseph Mbilinyi |
Na: Frank Sanga na Anthony Kayanda, Kigoma, MWANANCHI.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais. Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma. Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.
“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi. “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.
“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu. “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.” Atangaza kugombea urais Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.
Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye na Mwananchi kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”
“Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka 51 mpaka 46. Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.
“Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.
“CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto. Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

MAMBA MZITO ZAIDI MAREKANI ANASWA
Mamba aliyekamatwa Mississippi |
MAMBA mwenye uzito wa kg. 316
amenaswa kufuatia juhudi ya kumsaka iliyofanywa na watu wanne kwenye
ranchi ya Mississippi nchini Marekani na ameweka rekodi ya kuwa mamba
mzito zaidi nchini humo.
Eneo la chini la Mississippi Delta linahusisha klabu nyingi za uwindaji, ardhi ya mbao, kilimo na maeneo ya hifadhi za wanyama.
Rekodi ya awali nchini humo ilikuwa ni mamba mwenye uzito wa kg. 312 na alikamatwa mwaka jana kwenye maji hayo hayo ya Delta.
Mamba huyo ana urefu wa futi 13 na inchi 1.5.
Hata hivyo, rekodi rasmi za mamba wakubwa zaidi duniani zinashikiliwa na mamba wawili wenye urefu wa futi 20 (mita 6.2) na kg 1,200.
Mamba wa kwanza aliuawa Mto Mary kaskazini mwa Australia mwaka 1974 na kupimwa na maafisa wa wanyama. Mamba wa pili aliuawa mwaka 1983 katika Mto Fly, Papua New Guinea. Katika suala la mamba wa pili, kilichopimwa kilikuwa ni ngozi ya mamba huyo na inafahamika kwamba ngozi pekee huwa inatoa vipimo pungufu vya urefu halisi wa mnyama, hivyo mambo huyo inawezkana alikuwa na urefu wa sentimeta 10 zaidi.
LEMA AFURAHIA KESI YAKE KUSIKILIZWA NA JAJI MKUUEneo la chini la Mississippi Delta linahusisha klabu nyingi za uwindaji, ardhi ya mbao, kilimo na maeneo ya hifadhi za wanyama.
Rekodi ya awali nchini humo ilikuwa ni mamba mwenye uzito wa kg. 312 na alikamatwa mwaka jana kwenye maji hayo hayo ya Delta.
Mamba huyo ana urefu wa futi 13 na inchi 1.5.
Hata hivyo, rekodi rasmi za mamba wakubwa zaidi duniani zinashikiliwa na mamba wawili wenye urefu wa futi 20 (mita 6.2) na kg 1,200.
Mamba wa kwanza aliuawa Mto Mary kaskazini mwa Australia mwaka 1974 na kupimwa na maafisa wa wanyama. Mamba wa pili aliuawa mwaka 1983 katika Mto Fly, Papua New Guinea. Katika suala la mamba wa pili, kilichopimwa kilikuwa ni ngozi ya mamba huyo na inafahamika kwamba ngozi pekee huwa inatoa vipimo pungufu vya urefu halisi wa mnyama, hivyo mambo huyo inawezkana alikuwa na urefu wa sentimeta 10 zaidi.
Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Othman Chande |
Godbless Lema |
Akizungumza katika mahojiano yake leo na kituo cha redio cha Clouds FM kupitia kipindi cha Bongo Amplifanya, Lema amesema kuwa yeye binafsi hataki kupendelewa bali haki itendeke na kwamba anaamini kuwa uamuzi wa jopo la majaji wa Mahakama ya Rufaa litakaloongozwa na Jaji Chande utakuwa ni wa haki na yuko tayari kuupokea.
"Sitaki upendeleo, nipendelewa nitaogopa, nitalia... niko tayari kurudi kwenye uchaguzi, na ninaamini nitashinda kwa idadi ya kura za kubebwa kwenye canter.... nimefurahi kuwa kesi hii itaongozwa na Jaji Mkuu Chande," amesema.
'Yeye (Chande) ndiyo mkuu wa mahakama... ninaamini vipengele vitapitiwa kwa haki," amesema Lema ambaye ubunge wake ulitenguliwa na mahakama kutokana na kasoro kadhaa na hivyo akakata rufaa kupinga uamuzi huo
MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA
KIKAO CHA NEC YA CCM KINACHOENDELEA DODOMA
JK ASEMA ANAYETAKA KUONDOKA CCM RUKSA
NI WALE WANAOTISHIA BAADA YA KUTOSWA, AWASHANGAA WANAOTISHIANA SILAHA KWA AJILI YA UONGOZI
Na: Midraji Ibrahim na Habel Chidawali, Mwananchi MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amewatolea uvivu wagombea wa nafasi mbalimbali ambao majina yao yamekatwa, akisema wanaotaka kukihama chama hicho kwa sababu wametoswa, waondoke haraka. Licha ya kuwatakia safari njema, Rais Kikwete aliwatupia lawama baadhi ya wanaCCM ambao wameripotiwa kuendesha malumbano na kugeuza uchaguzi huo kama uwanja wa vita. Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) jana, Rais Kikwete alisema kumekuwapo na taarifa mbalimbali ambazo zimemfikia pia kwamba baadhi ya wanachama wanatishia kukihama chama hicho kama majina yao yatakatwa. “Wako wenye ndimi mbili ambao wanasema kuwa wasipoteuliwa wanaweza kuondoka. Ah! Mimi nasema watangulie huko maana inaonyesha kuwa walishaandaa maeneo ya kwenda,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wajumbe wa Nec. Alisema CCM kinayo taarifa kuhusu watu kugombana na hata kutoleana silaha, jambo alilosema linashangaza, huku akihoji kuna nini katika uongozi tena Nec? “Uchaguzi usigeuzwe uwanja wa fujo.
Wengine wanatoleana silaha kama majembe, ngumi na silaha nyingine, hivi wanagombana nini huko? Uchaguzi usigeuzwe kuwa ni uwanja wa vita.” alisema. Hivi karibuni, baadhi ya makada wa chama hicho wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali za kukitishia chama hicho akiwemo Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye alikaririwa akisema kama jina lake halitapitishwa, patachimbika. Mbunge huyo alisema hayo siku chache baada ya jina lake kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi iliyokuwa ikipitia na kuteua wagombea watatu kwa ajili ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
"Hapatatosha CCM," alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali. Ingawa Rais Kikwete hakutaja majina, Mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangallah na Hussein Bashe nao waliripotiwa kutoleana maneno makali hata kuonyeshana bastola, huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli wakiendesha malumbano kwa muda mrefu. Inadaiwa kuwa majina hayo yote na ya vigogo wengine yamekatwa na jana baadhi yao walikuwa wanadai kuwa CCM kinataka kuzalisha upinzani ambao utakisababishia kushindwa katika safari yake kisiasa hasa katika mfumo huu wa vyama vingi. Licha ya makaripio hayo, Rais Kikwete alibainisha kuwa CCM kinasemwa na watu kuwa kinakithiri rushwa katika chaguzi zake hivyo akawataka wagombea kubadilika kabla ya kukamatwa na Takukuru. “Zipo taarifa ingawa hatujazithibitisha kwamba wapo baadhi ya wagombea wanamwaga fedha sijawahi kuona… Takukuru wapo wanaendelea na kazi. Chama chetu kinasemwa tujipe fursa ya kubadilika, tusisubiri kukamatwa na kuanza kuilaumu PCCB.”
Kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, Rais Kikwete alisema katika uchaguzi huo, wamejitokeza watu wengi tena vijana wasomi na kwamba Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu, zimewapandisha na kuwakata waliotumikia chama muda mrefu. “Kama hukuteuliwa kuna mawili, ama nafasi zimejaa au hufai una upungufu kidogo na huo ni utaratibu wa chama siyo kuoneana,” alisema Rais Kikwete huku akishangiliwa.
Alisema katika uteuzi huo vijana watapewa nafasi zaidi kutokana na ukweli kuwa, chama bila ya vijana hakiwezi kuwa imara kwa sababu ndiyo nguvu ya ushindi. “Hao watakaoachwa watambue kuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza timu ya ushindi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa Bara na Visiwani, hivyo kuachwa jina lako isiwe nongwa,” alisema na kuongeza: “Lazima tukipe chama chetu watu wa kushinda… Lazima tutambue sasa tunaunda timu ya ushindi wa chama siyo ushindi wa mtu.” Hata hivyo, Rais Kikwete alitoa angalizo kuwa anajua kikao cha Halmashauri Kuu kingekuwa na mjadala mzito, lakini lazima wakipe chama watu wa kushinda. Majina manne Kamati Kuu ya CCM, inadaiwa kupendekeza majina ya wagombea wanne kwenye jumuiya zake, tofauti na kanuni ya chama hicho ya nafasi moja kuwaniwa na watu watatu. Kikao chake kilichomalizika juzi usiku, kinadaiwa kubadili kanuni ya kupendekeza wagombea watatu kwa nafasi moja na kwamba, hivi sasa mapendekezo hasa kwenye jumuiya ni wagombea wanne.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa, hatua hiyo inalenga kutoa ushindani kwa wagombea. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipotakiwa kuzungumzia suala hilo hakukanusha wala kukubali zaidi ya kusema kwamba hata kama utaratibu huo umetumika siyo mara ya kwanza kwa chama hicho. Alisema kama Jumuiya ya Vijana wanaojitokeza lengo lao linakuwa kupata uzoefu na kwamba, idadi ya majina inategemeana na busara za kikao kinavyoona ili kutoa nafasi kwa wagombea kujipima. Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz
UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI UNAVYOENDELEA ENEO LA KIMARA-MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM LEO SEPT 26, 2012
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema akihutubia |
Mhe. Lema akiwa na Mhe. Joshua Nassari |
Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe.Joshua Nassari akihutubia |
Kada aliyejitoa CCM Arusha Ally Bananga |

CHADEMA KATIKA KESI YA ALIYEKUWA MBUNGE WA ARUSHA MJINI Mh GODBLESS LEMA
Gari ya polisi ikiwa imepaki pembeni kupisha maandamano ya wafuasi wa CHADEMA |
Wafuasi wa CHADEMA wakielekea katika ofisi za chama |
Msafara wa wafuasi wa CHADEMA wakitokea mahakamani kuelekea ofisi za chama hicho |
Gari alilopanda aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA)Godbless Lema likiwa linasukumwa na wafuasi wa chama hicho mara baada ya kutoka mahakamani |
Aliyekuwa
Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Mh Godbless Lema akiongea na wananchi nje
ya ofisi ya chama mara baada ya kutoka mahakamani |
Wananchi wakiwa nje ya ofisi ya CHADEMA wanamsikiliza aliyekua mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless lema |
RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI
UJENZI UNAVYOENDELEA BARABARA YA MOROGORO (MOROGORO ROAD) ENEO LA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM
BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA) TAIFA WAKUTANA MOROGORO KWA AJILI YA KUWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA CHAMA
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakipitia ajenda za kikao |
Wajumbe wakisimama kwa muda mfupi kuwakumbuka waliopoteza maisha |
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche akifungua kikao |
KWA HABARI HII YA UTABIRI WA HALI YA HEWA (MVUA INAYOTARAJIWA KUNYESHA KARIBUNI),SIJUI DAR ES SALAAM ITAKUWAJE MAENEO YA MABONDENI KAMA HAYA!
HAPA NI ENEO LA KIMARA MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM
RAIS KIKWETE AZINDUA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA,KUNDUCHI JIJINI DA ES SALAAM
Baadhi ya wanafunzi wa kwanza wa Chuo hicho, wakitoa heshima zao kwa Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi huo leo. |
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kwanza wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, mara baada ya kukizindua, Dar es Salaam leo. |
MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI DAR LEO
PICHA ZA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI UNAOENDELEA BARABARA YA MOROGORO (MOROGORO ROAD) KATIKA ENEO LA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment