MAGAZETI YASEMAVYO LEO
IJUMAA OCT 25, 2013
JUMANNE OCT 02, 2012
JUMATATU OCT 01, 2012
JUMAMOSI SEPT 29, 2012
IJUMAA SEPT 28, 2012
ALHAMISI SEPT 27, 2012
JUMATANO SEPT 26, 2012
JUMANNE SEPT 25, 2012
JUMATATU SEPT 24 2012
WANAFUNZI VYUO VIKUU WAKUMBWA NA WASIWASI WA KUPATA MIKOPO
IJUMAA OCT 25, 2013
JUMANNE OCT 02, 2012
JUMATATU OCT 01, 2012
JUMAMOSI SEPT 29, 2012
IJUMAA SEPT 28, 2012
ALHAMISI SEPT 27, 2012
JUMATANO SEPT 26, 2012
JUMANNE SEPT 25, 2012
JUMATATU SEPT 24 2012
WANAFUNZI VYUO VIKUU WAKUMBWA NA WASIWASI WA KUPATA MIKOPO
Wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu nchini, wako hatarini kuchelewa kupata fedha
za mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
kutokana na mchakato wa kutoa mikopo hiyo kuchelewa kuanza.Hali hiyo inatokana na vyuo hivyo kuanza kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao.
Uchunguzi
uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa wanafunzi katika vyuo hivyo
walioomba mikopo toka HESLB, bado hawajaanza kupata hatua ambayo imeanza
kuwapa shaka kama wataripoti vyuoni kwa wakati kutokana na kutegemea
fedha za mikopo kwa ajili ya ada ya masomo na mahitaji mengine.
Kutokana
na ucheleweshaji wa mikopo hiyo, gazeti hili lilishudia wanafunzi
kadhaa ambao wamedahiliwa kujiunga vyuo vya elimu ya juu mwaka huu,
wakimiminika katika ofisi za HESLB makao makuu jijini Dar es Salaam
kuulizia hatma ya mikopo waliyoomba.
“Unavyoniona
hapa ni wiki ya tatu nimekuwa nikija hapa ofisi za Bodi ya Mikopo
kuulizia kama mikopo imeanza kutolewa, lakini tunaelezwa tuendelee
kusubiri wakati vyuo vimekaribia kufunguliwa,” alisema mwanafunzi mmoja
aliyetoka Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
Hata
hivyo, Afisa mmoja wa HESLB, aliyejitambulisha kwa jina moja la
Venelanda, alisema mchakato wa kuandaa mikopo ya wanafunzi bado
unaendelea na kwamba zoezi hilo linachukua muda kidogo kutokana na
mikopo hadi kukamilika kwake hupitia maeneo mengi.
Venelanda
ambaye hata hivyo, hakutoa jibu la moja kwa moja kama mikopo kwa
wanafunzi hao itaanza kutolewa lini, alisema HESLB itahakikisha mikopo
hiyo inatolewa kwa wanafunzi hao kabla ya kufunguliwa vyuo hivyo.
Mkuu
wa Idara ya Habari Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, alipoulizwa na
gazeti hili kama fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu
zimeshapelekwa HESLB, alisema suala hilo waulizwe Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
“Bajeti
ikishapitishwa bungeni, kinachobakia ni kwa wizara husika kushughulikia
mipango yake, hivyo hata suala la fedha za mikopo ya wanafunzi wa vyuo
vikuu wenye majibu ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,” alisema
Mduma.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo, alipoulizwa na
NIPASHE, alisema kimsingi mikopo bado haijaanza kutolewa kwa wanafunzi
wa vyuo vya elimu ya juu na kufafanua kuwa kuanzia wiki hii wizara yake
itaangalia uwezekano wa kushughulikia suala hilo ili wahusika wapewe
mikopo hiyo.Rais
wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso),
Bhokombe Itembe, alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanatarajia
kuripoti chuoni hapo Oktoba Mosi, mwaka huu.Alisema
wiki iliyopita uongozi wa chuo na Daruso, walitaka kupanga vyumba
katika hosteli kwa ajili ya wanafunzi, lakini zoezi hilo lilishindikana
kwa sababu bado haijafahamika idadi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza
watakaoripoti chuoni hapo.Itembe
alisema tatizo la kuchelewa kwa mikopo linatokana na sababu kadhaa,
ikiwemo kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya HESLB na Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania (TCU).“Mwanafunzi
anapodahiliwa bila TCU kumuamulia ataenda chuo gani, huwezi kwenda na
wakati huo huo bila HESLB kukupatia mkopo, vile vile huwezi kwenda
chuoni,” alisema Itembe.Rais
wa Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha IFM, Michael Chazy, alisema chuo
hicho kitafunguliwa Oktoba 8, mwaka huu na kwamba hadi sasa bado
wanafunzi wanaoendelea na wale wa mwaka wa kwanza hawajaanza kupatiwa
mikopo.Naye
Rais wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Paul Yunge, alisema suala la
mikopo katika chuo lina utata hasa kwa wanafunzi wanaoanza mwaka wa
kwanza ambapo baadhi yao wamejaza fomu vibaya na hivyo taasisi husika
zinashughulikia tatizo hilo.Rais
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Amos Chakushemeire, alisema utoaji wa mikopo
hauridhishi kabisa katika chuo hicho ambapo wanafunzi walioanza muhula
Julai, mwaka huu, wamelipwa robo ya mkopo wakati kiasi kingine cha mkopo
hawajalipwa hadi sasa, hali ambayo imesababisha ukata mkubwa kwa
wanafunzi.“Chuo
chetu ni tofauti na vingine, kina mihula mitatu, wanafunzi walioanza
muhula wa Julai hawajalipwa sehemu nyingine,. Hivi karibuni uongozi wa
chuo ulilazimika kuwakopesha Sh. 50,000 wanachuo hao ili kuwatuliza
wasigome,” alisema Chakushemeire.Rais
wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Frank Nkinda, alisema mikopo ni changamoto
kubwa katika chuo hicho ambapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawajapata
mikopo hadi sasa.Alisema
kutokana na hali hiyo, hivi karibu Mwenyekiti wa HESLB alifika chuoni
hapo kuzungumza na uongozi, serikali ya wanafunzi na wanachuo ambapo
alitoa ahadi kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika mwaka
huu wa 2012/2013.Mwaka
jana serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza
utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo ambapo badala ya fedha hizo kutolewa
kwa waombaji na HESLB, sasa fedha hizo zinapelekwa vyuoni ambako
menejimenti za vyuo zinawajibika kuzisimamia na kuwapa waombaji.Hatua
hiyo ilifikiwa ili kurahisisha mchakato wa kuwapatia fedha waombaji na
pia kuepusha usumbufu kwa HESLB kutokana na wanafunzi kutoka vyuoni
kuvamia ofisi hizo kwa lengo la kushinikiza wapewe fedha.Taarifa
iliyotolewa na HESLB na TCU Agosti 10 na 12, mwaka huu ilieleza kuwa
zaidi ya wanafunzi 3,074 walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka
2012/13, wameenguliwa katika maombi yao kutokana na dosari mbalimbali.Taarifa
hiyo ilieleza kuwa HESLB pekee iliorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649
ambao ilibaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa
mikopo.Miongoni
mwa makosa ama dosari ambazo HESLB ilizibaini kwa walioenguliwa ni
pamoja na kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya
mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini,
kukosekana kwa sahihi za viongozi wa serikali za mitaa/vijiji kwa
waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.Kwa upande wake TCU, iliwaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali.Miongoni
mwa dosari ambazo zilitajwa na TCU ni pamoja na baadhi yao kukosea
namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano, miaka ya kumaliza
masomo, mawasiliano sahihi kwa muombaji pamoja na uchaguzi wa masomo.Hata
hivyo, taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana
na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao
kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa.Kwa mwaka huu wa fedha 2012/13, serikali imeiongezea fedha HESLB kwa kuitengea Sh. bilioni 326 kwa wanafunzi 98,772.Mwaka jana, serikali iliitengea HESLB Sh. 91,722,783,264 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.Ucheleweshaji
wa fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umekuwa ukisababisha
wafanye migomo, vurugu na maandamano mara kwa mara kushinikiza walipwe.
NA THOBIAS MWANAKATWE
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment