Prof R. MUKANDARA:WANAFUNZI WENGI WA KITANZANIA HUKIMBIA SOMO LA HESABU WAFIKAPO VYUO VYA ELIMU YA JUU
|
Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof Rwakaza Mukandara |
Tanzania ina wanafunzi wengi wenye uwezo mkubwa katika somo la Hisabati wawapo katinga ngazi ya shule za msingi na sekondari lakini hupotea kabisa pindi wafikapo katika masomo ya elimu ya juu.Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam Prof Rwekaza Mukandara alieleza kuwa wanafunzi wengi wafikapo elimu ya juu huachana na fani za hesabu na sayansi na kuchagua fani za sanaa na biashara ili watakapohitimu wapate soko la ajira lenye faida."Wengi wamekuwa wakiamini kuwa hesabu haiwezi kuwahakikishia ajira wanapomaliza chuo kwahiyo hubadili pindi wajiungapo na masomo ya elimu ya juu" alisema Profesa Mukandara katika mkutano wa Africa Mashariki juu ya Programu ya Hesabu (East Africa Universities Mathematics Programme
(EAUMP) Conference) uliofanyika katika Taasisi ya Sayansi na Technolojia ya Nelson Mandela.
No comments:
Post a Comment